islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


KUMTEGEMEA NA MWEYEZI MUNGU


11858
wasifu
Kumpenda Mwenyezi Mngu na Mtume Wake ni miongoni mambo ya Imani ya lazima. Mtu hawi Muislamu mwenye Imani mpaka atangulize mapenzi ya Mwenyezi Mngu na Mtume Wake mbele ya kila alichonacho, kiwe ni mali, mtoto, mzazi au watu wote, kama alivyoeleza Mpendwa Mteuliwa, rehema na amani zimshukie. Na kwa kadiri ya mapenzi ndiounapatikana utiifu na kufuata amri ya Mwenyezi Mngu na Mtume Wake, rehema na amani zimshukie.
Khutba ya

Namshukuru Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Ambae wanamtegemea yeye wenye kumtegemea, Aliyesema mwenye kumtegemea yeye anamtosha. Sala na Salamu zimshukie Mtume Muhammad, Mtume wa mwisho na Jamaa zake na Sahaba zake wote..

Kutegemea imechukuliwa katika neno (wakala) kama kusema fulani amelitegemeza jambo lake kwa fulani na akamtegemea yeye. Kwa hivyo, kutegemea ni tafsiri ya kutegemea kwa mwenye kutegemewa, na wala hamtegemei mwanadamu mtu mwingine ila anaitakidi kwake kupata jambo.

Enyi wasikilizaji, kutafuta riziki ni maumbile ya kila mwanadamu. Utaona kukipambazuka mwanadamu anakwenda mbio, kwa sababu ya kutafuta riziki. Mkulima anajiandaa kwenda shambani. Mfanya biashara ajiandaa kwenda kwenye biashara yake. Kila mja hujiandaa kivyake. Na wote wanapata shida kwa sababu kila mmoja anataka kuhifadhi na kupata chakula cha yule anayemlazimu kumlisha; mke, watoto ama chakula cha familia yake.

Na hakika kuwa na himaya ya kutafuta cha kutosheleza au kutaka utajiri pamoja na kuwa njia yake ina vikwazo na safari ndefu. Yote hayo hupelekea lawama. Enyi Waja Dini ya kiislamu inakataa ya kwamba riziki inapatikana kwa njia ya udanganyifu. Na inakataza na kuchukia Muislamu kuitegemea njia hiyo ili apate riziki kutokana nayo. Na katika kuziba mlangu huu na njia hii. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Isiwepelekeeni nyinyi uzito wa kupata riziki mukaingia katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Hazipatikani zilizoko kwa Mwenyezi Mungu ila kwa Twaa yake].

Kwa hivyo, ni yapi mapitio? Na nini suluhisho kutokana na maisha haya wanaoishi, watu wanatusiana, baadhi yao wanakula nguvu za wengine na baadhi yao kuwadhulumu baadhi. Na katika zama zetu hizi tunazoishi tunashuhudia hayo na kuna mifano mingi.

Enyi Waislam isikilizeni Hadithi hii inayotoka kwa Mtume wenu Muhammad, ikipokewa na ‘Umar Bin Khatwab Akisema: “Nimemsikia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: Lau hakika nyinyi mungalikuwa munamtegemea Mwenyezi Mungu haki ya kumtegemea, Angaliwaruzuku nyinyi kama anavyowaruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa, na anarudi jioni akiwa ameshiba”. Kutokana na hadithi hii tunajifunza ya kwamba tukimtegemea Mwenyezi Mungu kikweli basi Mwenyezi Mungu atatupa tunalolitaka.

Enyi Waislamu watukufu, zimekuja Aya nyingi na Hadithi nyingi zilizo sahihi kubainisha kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa kila jambo letu na katika maisha yetu yote. Na hakika kumtegemea Mwenyezi Mungu ni jambo kubwa na ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu akiwaamrisha waja wake Waislamu. Amewaamrisha hilo kwa hali zote. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال تعالى : (وَلِلَّهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ )[هود: 123]

{{Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyofichika mbinguni na ardhini na mambo yote yanarejeshwa kwake na hakuwa Mola wako mwenye kughafilika na munayoyatenda}} [Huud : 123). Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال تعالى: (وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ وَكَفَى بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا) [الفرقان: 58]

{{Mtegemeni Mwenyezi Mungu wa milele, Ambae hafi na mtukuze Mola wako naye anatosha kwa dhambi za waja wake anazijua}} [ Al-Furqan : 58].

وقال تعالى) : وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ) [الشعراء: 217]

{{Na umtegemee Mola wako mwenye nguvu mwenye rehema}} [Shuaraa : 217].

وقال : (وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ وَكِيلًا) [الأحزاب: 3]

{{Na umtegemee Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atosha kuwa mlinzi}} [Ahzaab : 3].

Na katika Hadithi ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) inatuelezea kuhusu kumtegemea Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Imetokana na Abu Hurayra radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie Akipokea kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Wataingia peponi watu nyoyo zao ni mfano wa nyoyo za ndege] (Muslim). Maana yake wanaomtegemea Mwenyezi Mungu na kumesemwa nyoyo zao ni laini.

Enyi Ndugu, Hakika kutegemea ni kusadikisha kutegemea moyo kwa Mwenyezi Mungu katika kuleta mambo mema na kuondosha madhara. Vilevile kumtegemea Mwenyezi Mungu ni ukweli na imani na utulivu na kua na mafungamano baina ya mja na Mola wake.

Amesema Ibnul-Qayyim amrehemu yeye Mwenyezi Mungu: “Kutegemea ni nusu ya imani na ni nusu ya pili ya kurudi kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaahidi wenye kumtegemea malipo makubwa na malipo mengi”. Katika Hadithi iliyoko katika sahihi mbili hadithi ya watu sabini elfu wataingia peponi bila hisabu, nao ni wale ambao hawataki kuzunguliwa, wala hawajichomi, wala hawatabiri ndege wanamtegemea Mola wao”.

Na hakukuwa kutegemea Mwenyezi Mungu kunakanusha kuchukua sababu za sheria zilizo halali. Mfano mtu akisema mimi sitafuti riziki wala siendei mbio, ikiwa imeandikwa kwangu niwe tajiri nitakuwa tajiri bila kutaabika wala shida, ikiwa SIkuandikiwa basi siwi hakuna haja nisumbuke wala nipate taabu. Kwahivyo, linalotakiwa ni kumtegemea Mwenyezi Mungu pamoja na kufuata sababu.

Na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amewasifu wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa sifa mbili:

Kwenda kutafuta riziki.

kutegemea sababu za kisheria.

Mwenye kukosa moja wa sifa mbili hizi hakika ameangukia patupu na amefanya shirki. Na mwenye kwenda kwa sababu zilizo halali na akamtegemea mola wake na akamshukuru mola kwa kila yanayopendeza na akasubiri hukumu ya Mwenyezi Mungu wakati anapopata msiba na machukivu amefaulu na amefadhilisha ukamilifu wote.

Khutba ya pili

Enyi Waislamu hakika kutegemea ni kuusadikisha moyo juu ya kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kuleta mambo mema na kujihami na madhara. Na kujua ya kuwa hapana yoyote anayeweza kukunufaisha na kitu chochote ila kile alicho kupangia Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Vile vile kutegemea ni ukweli na imani na utulivu na kuwa na uaminifu na Mwenyezi Mungu na matarajo yanayo shikamana na vitendo vizima ambavyo hauzimiki mwangaza wake japo yanapatikana matatizo.

Amesema Ibnul- Qayyim amrehemu yeye Mwenyezi Mungu: ‘Kutegemea ni nusu ya imani na nusu ya pili ni kurudi kwa Mwenyezi Mungu’. Na haikuwa kutegemea inamzuia mwanadamu kutafuta sababu ya kisharia iliyo ya halali. Watu wema wanasema: Wakati unapo fanya bidii kutafuta riziki, na kumtegemea Mwenyezi Mungu utapata njia ya ya kila kheri. Na jambo kubwa linalo pelekea kumtegemea Mwenyezi Mungu, ni kumjua Mwenyezi Mungu kwa majina yake na sifa zake na kumpwekesha yeye Alie takasika.

Enyi Waislamu, Maajabu ni kwa yule anaye jua kuwa yeye ni muhitaji kwa Mola wake kwa kila hali zake kisha hamtegemei Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Hakika mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu anamtosha. Na mwenye kumtaka msaada Mwenyezi Mungu humtengenezea Dini yake na Dunia yake. Na mwenye kujiona na nafsi yake na ukakatika moyo wake na Mola wake ameangamia na ameangukia patupu.

Na hakuna kufaulu wala kupata furaha ila kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuomba msaada kwake. Yeye ndie mwenye kuabudiwa kiukweli, na yeye anastahiki kuombwa msaada peke yake.

Mwisho

Mwenyezi Mungu atujaalie ni wenye kumtegemea yeye peke yake, na tusimshirikishe na chochote. Atujaaliye ni wenye kusikia pamoja na kufuata na Atuoneshe batili aturuzuku kuiepuka, Atupe mema ya ulimwenguni na akhera.





Vitambulisho: