islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


mnasaba wa mwaka mpua


7166
wasifu
Siku zinapita na miaka yaenda mbio. Miongoni watu kuna wanao jikurubisha kwa mwenyezi mungu kwa ibada, na kuna wengine wanao jiweka mbali nayeye. Na kila mwaka ukimpita mtu, unatoa ushahidi kwa maslahi yake au dhidi yake. Basi mwenye akili ni Yule anayechukua fursa ya umri wake na akafaidika na wakati wake kwa kumridhisha Allah (SW) na kufanya kazi kwa bidii yenye kuleta matunda ya kunufuisha Dini yake na Jamii yake.
Khutba ya

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Swala na salamu zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Inapaswa kwa kila mwanadamu kujiuliza maswala haya:-

Nimekuja kutoka wapi?

Naenda wapi?

Ulimwengu huu ulioko pembezoni mwangu umekuja kutoka wapi?

Kwa ajili gani nimeumbwa?

Matamanio ni sababu ya mtu kujisahau, na kumalizika mwaka kwa haraka, amesema Hassan Basri: Tahadharini na matamanio, kwani hapati mtu na tamanio kheri ya duniani na kesho akhera. Mafhumu Neno lake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :

قال الله تعالى :(أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ )[التوبة: 126]

{{Je, Hawaoni ya kwamba wanatiwa mitihani kila mwaka mara moja au mara mbili au zaidi. Kisha hawatubu wala hawakumbuki}}. Amesema Mujaahid: wataonjwa kwa ukame na njaa. Amesema Qatada: wataonjwa kwa kupigana vita mara moja na mara mbili. Amesema Mujaahid: wataonjwa kwa ukame na shida. Amesema ‘Atwiyyah: Wataonjwa kwa maradhi na maumivu.

Maswali muhimu yanapaswa kwa mwanadamu kujibu. Maswali hayo baada ya kumalizika kwa mwaka. Kila mwanadamu anapaswa kujiuliza maswali haya:-

Swala ngapi hukuswali?

Umepuuza jumaa ngapi?

Saumu ngapi hukufunga?

Mali ngapi hukuyatolea zaka?

Hija ngapi zimekupita?

Umefanyia uvivu wema ngapi?

Uovu kiasi gani uliounyamazia?

Mambo mangapi ya haramu umeyaangalia?

Maneno mangapi machafu umeyazungumza?

Mara ngapi umewaudhi wazazi wako wawili na wala hukuwaridhisha?

Umewavisha madhaifu wangapi?

Wangapi umewadhulumu?

Umuhimu wa Wakati

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنْظُرْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ )[الحشر: 18]

{{Enyi mlioamini, Mcheni Mwenyezi Mungu; na kila mtu aangalie anayoyatanguliza kwa ajili ya kesho (Akhera); na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu Anazo habari za mnayoyatenda yote}}.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِنْ سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا( [آل عمران: 30] {{Siku ambayo kila nafsi itakuta mema iliyoyafanya yamehudhurishwa, na pia ubaya ilioufanya. Itapenda lau kungekuwa na masafa marefu baina ya ubaya huo na yeye}}. Amesema ‘Umar: ‘ Hesabuni nafsi zenu kabla hazijahisabiwa na pimeni nafsi zenu kabla hazijapimwa, kwani itakuwa ni wepesi kwenu nyinyi siku ya Qiyama ikiwa mtahesabu nafsi zenu.

Ndugu Waislamu, Je tumejiandaa kiasi gani kwenda kujibu maswali mbele ya Allah siku ya kiama?. Kila moja ajiulize suala hilo na aandae jibu la ukweli kabisa. Kwasababu kuokoka mwanadamu siku hiyo, ni kujibu swali atakalo ulizwa na Allah siku ya hesabu.

Mfano Mzuri wa Kuhesabu Nafsi

Abubakar alikuwa akiuzuia ulimi wake ukitoka nje, na akisema: kiungo hiki kimeniingiza katika maangamivu.

Amesema Ghunaym: tulikuwa tukijipatia mawaidha kwa mambo mane:

Fanya amali njema katika ujana wako kabla utu uzima

Unapokuwa na wakati kabla kuwa na shughuli

Unapokuwa na afya kbala kuwa mgonjwa

Unapokuwa hai kabla hujafa.

Khutba ya pili

Daraja za kuhesabu nafsi:-

Ibnu Qayyim ameelezea njia za kuhesabu nafsi:

Kufanya mambo ya faradhi, fatiliza ukiona kuna upungufu

Ukifanya maasi, fuatiliza kwa toba na kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha na kufanya amali njema.

Ukighafilika mtaje Mwenyezi Mungu

Kuhesabu nafsi viungo vyake, ni kujiuliza unataka nini? Na kwa njia gani umefanya?

Mambo Manne yenye Kunawirisha Moyo:

Amesema ‘Uthman Bin Fuudy: mambo manne yenye kunawirisha moyo:

Kumcha Mwenyezi Mungu

Kusoma Qur’an.

Kusoma Hadithi za Mtume na sera zake.

Kujishughulisha na waja wema waliotangulia.

Amesema Ibrahim Nukhaiy: ‘Ewe Mwenyezi Mungu, tuhifadhi na kitabu chako, na Sunnah ya Mtume wako, na tulinde kufuata matamanio, na njia iliyopotea na shubuhaat katika mambo, na dhulma na malumbano’.

Mwisho

Mwaka mpya ni neema kubwa kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Taala) na wakati huo huo neema hii inaweza ikabadilika na ikawa ni adhabu na mitihani mikubwa kwa mwanadamu. La msingi ni Muislamu kufuata maamrisho ya Allah (Subhaanahu wa Taala) na kushikamana na Sunnah ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Kufanya hivyo, ndio mwaka wako utakuwa ni mwaka wa neema nyingi. Kinyume na hayo, mwaka wako utakuwa ni adhabu na mitihani na misukosuko mbali mbali ya kilimwengu..

Tumuombe Mwenyezi Mungu Atusamehe madhambi yetu yaliopita na Atuwezeshe kufanya amali njema katika mwaka huu mpya, na Atuteremshie baraka na neema katika mwaka huu mpya.





Vitambulisho: