islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


njia za kuvuta nyoyo za watu


5194
wasifu
Kuamiliana na nyoyo ili kuzivuta ni ujuzi unaohitaji mtu auelewe vizuri. Na mtu anayetaka kufaulu katika kuamiliana na nyoyo hana budi ajue funguo na lugha ya nyoyo, na awe na yakini kuwa kila moyo una ufunguo wake ambao bila ya ufunguo huo hataweza kuingia kwenye moyo huo. Miongoni mwa hizo ni kutabasamu, kunza kupiga salamu, kupa tunu na mfano wa hayo.
Khutba ya

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote, na rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad. Moyo ni kiungo muhimu katika mwili wa mwanadamu. Moyo ukiwa mzuri, mwili utakuwa mzuri. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Katika mwili wa mwanadamu kuna kipande cha nyama, kikiwa kizuri, basi mwili wote unakuwa mzuri. Na kikiwa kibaya mwili wote unakuwa mbaya. Jueni ni moyo].

Kinyume na hayo, ni moyo kuwa nasifa ya ngumu, na kusababisha kupinga na kukata haki.

Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): فَأَمَّا الْإِنْسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ) [الفجر: 15]

{{Hakika, ama mwanaadamu Mola wake atakapofanyia mtihani akamtukuza kwakumneemesha,basi atasema: Mola wangu amenitukuza}}.

Na neno lake Allah (Subhaanahu wa Taala):

قوله تعالى) وَلَئِنْ أَذَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَاهَا مِنْهُ إِنَّهُ لَيَئُوسٌ كَفُورٌ9 وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ نَعْمَاءَ بَعْدَ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ السَّيِّئَاتُ عَنِّي إِنَّهُ لَفَرِحٌ فَخُورٌ10 إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَئِكَ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ) [هود: 11]

 

{{Na Wallahi tutakapomneesha mwanaadamu kwa neema yoyote kisha tukamwondoshea hapana shaka Yeye ni mwingi wa kukata tamaa, mwenye kukanusha. Na Wallahi tutakapomneemesha baada ya kupata madhara Wallahi, atasema; imeniondokea mimi shida hapana shaka yeye ni mwingi wa furaha,mwenye kujivuna. Ila walio subiri na wakafanya amali nzuri, hao wanamsamaha wa madhambi yao na malipo makubwa}}.

Katika maudhui yetu ya leo tutazungumzia kuhusu namna gani nyoyo zinavutiwa kwa kufanyiwa mambo ya kheri na kupendelea zaidi kufika katika machumo ya kufaulu kwa haraka.

Hima ya Uislamu katika Njia za Kuzifikia Nyoyo zote na Kuziunganisha

Neno la bibi khadija katika kusifu kwake tabia za bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : ‘Hakika wewe unaunga jamaa Na udugu alioufungumanisha bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kwa baadhi ya maswahaba zake. Na linashuhuduliwa vile vile kwa hadithi ya Jabir Ibn ‘Abdallah aliposema: “Tulikuwa katika jeshi wakagombana mtu katika muhajirina na mtu katika ansar, akasema huyu katika ansar «Enyi Maansar na akasema katika muhajirina «Enyi Muhajirina». Akalisikia jambo hilo Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema : [Bado hamujaacha mambo ya ujinga? Wakasema maswahaba wamekosana mtu katika Muhajirina na mtu katika Ansar Mtume Akasema uacheni (ujamaa na ukabila) hakika ni uvundo akasikia maneno haya ‘Abdallah ibn Ubayya akasema wamefanya hivyo, basi Wallahi tukirejea Madina atamtoa mwenye nguvu yule mnyonge. Maneno hayo yakamfikia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)].

Umar akasema: “Ewe Mtume wa Allah niache nikate shingo yake huyu mnafiki, akasema Mtume muache wasije watu wakasema ya kuwa Muhammad anawauwa maswahaba wake na walikuwa maansar ni wengi kuliko Muhajirina. Walipo kwenda Madina kisha Muhajirina wakawa wengi baadaye.» Ameitoa hadithi hiyo Bukhari na Muslim. Na anasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Enyi watu hakika miongoni mwenu mnakimbiza (fukuza watu) watu].

Kufungamanisha Nyenzo na Njia kwa Itikadi (Aqida) na Tabia.

Kupatikana kisa cha watu wa pango (as›habul kahfi) na kisa cha mtu aliyekuja kutoka mbali mpaka kwa Nabii Musa. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قوله تعالى) وَجَاءَ رَجُلٌ مِنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَى قَالَ يَا مُوسَى إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ20 فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ) [القصص: 21]

{{Na alikuja mwanamume kutoka (sehemu) ya mwisho wa mji akiwakimbia alisema: Ewe Musa, hapana shaka wakuu walifanya mpango ili wakuuwe. Basi utoke mji hapana shaka mimi kwako ni miongoni mwa wenye kukunasihi. Basi aliutoka mji ilhali ni mwenye khofu yuangalia (ni jambo gani litazuka). Alisema Ewe Mola wangu, niokoe na watu walio makafiri}}. Yote hayo ni kwa ajili ya kulinda mapenzi.

Sifa za Kimsingi

Ukweli wa kumuelekea Allah (Subhaanahu wa Taala) na kutafuta ilimu kwa njia ya Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na wema waliotangulia katika kuzivuta nyoyo. Yenye kutoa ushahidi wa hayo ni neno lake Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال الله تعالى: (فَبِمَا رَحْمَةٍ مِنَ اللَّهِ لِنْتَ لَهُمْ وَلَوْ كُنْتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانْفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ) [آل عمران: 159] ( {{Na lau ungelikuwa ni mkali, mgumu wa moyo basi wangelikukimbia walio pembeni (karibu) nawe}}.

Katika Aya nyingine Allah Alimuambia Mtume awasamehe na awaombee msamaha na awashauri katika mambo yote.

Baadhi za Njia za kuvutia Nyoyo:

Uso wa tabasamu.

Kupeana mikono.

Kusikiliza matatizo ya watu kwa uzuri

Kutoa nasaha nzuri.

Kutangamana na watu.

Kupenda kuwafikishia watu manufaa.

Kuwashajiisha na kuwasubiria watu mazito (wasiochukulika).

Kuwaondolea watu matatizo.

Kuinamisha macho.

Kujiepusha katika lisilowezekana.

Kufungamanisha hali ya matukio ya sasa na visa vya kweli katika Qur’an na Sunnah na habari za leo.

Kumshukuru na kutambua wenye kufanya mazuri (watendaji kheri).

Na ushahidi ya hayo, ni neno lake Allah (Subhaanahu wa Taala):

قوله تعالى: (وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ) [آل عمران: 134] {{Na wenye kuzizuia hasira zao, wenye kusamehe watu na Mwenyezi Mungu huwapenda wenye kufanya mema}}.

Na inashuhudia hadithi ambayo imetaja haki za Muislamu, na msaada wa Allah kwa mja atakapokuwa ni mwenye kumsaidia ndugu yake. Ibn ‘Umar amepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ya kwamba Amesema: [Muumini mwenye kutangamana na watu na anayesubiri maudhi yao ni bora kuliko muumini ambaye hatangamani na watu wala hasubiri maudhi yao].

Na imepokewa na Nuuman Ibn Bashiir amesema: Nimemsikia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akisema: [Mfano wa muumini katika mapenzi na huruma ni kama mfano wa kiwiliwili kimoja kitakapougua kiungo kimoja katika mwili vinashikwa na homa viungo vingine].

Khutba ya pili

Miongoni mwa njia ya kufungamanisha nyoyo ni kutekeleza haki za watu alizozitaja Bwana Mtume rehma na amani zimfikie katika hadithi, kutoa salamu, na kuwa na maneno mazuri na kulisha chakula, na kuitikia ualishi, na kusindikiza jeneza na kuliswalia na kuinamisha macho.

Imepokewa riwaya nyingine ya sifa hizo amepokea Abu Huraira kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Amesema: [Haki za Muislamu juu ya Muislamu mwenzake ni sita. Akaulizwa ni zipi (hizo haki) Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: ukikutana naye msalimie na akikualiaka itikia uwalishi wake na akichemua na kumshukuru Allah basi muombee rehma na akiwa mgonjwa mtembelee na akifa sindikiza jeneza lake].

Kuzijumuisha nyoyo na amali ya kufanya jamii na kufanya peke yako hiyo ndio makusudio..Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ( [المائدة: 2]

{{Na saidianeni kwa kufanya mema na kumcha Allah na wala msisaidiane katika madhambi na uadui}}.

Na neno lake Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : لَوْ أَنْفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ) [الأنفال: 63]

{{Lau ungetumia yaliyomo ardhini yote hungeweza kuunganisha nyoyo zao lakini Allah aliunganisha baina yao}}.

Mwisho

Ndugu Muislamu, kama tulivyo sikia katika khutbah, ni wajibu kwa walinganizi wa kiislamu kujipamba na sifa za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) katika kuwaita watu kufuata Dini ya Allah (Subhaanahu wa Taala). Tukitaka Da’wah yetu ifaulu na kufikia lengo la Da’wah, basi ni lazima Waislamu wote kusoma Sira (Maisha) ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na Mwasahaba. Kufanya hivyo, tutaweza kubadilisha ulimwengu mzima kama alivyo badilisha ulimwengu Mtume na Masahaba kwa kipindi kifupi.

Tunamuomba Allah Atupe uwezo wa kufahamu Sira ya Mtume na kuweza kuigiza katika maisha kwa jumla na katika Da’wah khaswa. Allah awanusuru Walinganizi wote katika njia yake.