islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


tabia ya ruhuma


7545
wasifu
uislamu ni dini inao amrisha watu kuhurumiana na kusikitikiana,na muislamu bora ni yule ambae atakuwa na ruhuma na ndugu zake waislamu.na mtume s.a.w ametuhimiza hilo akisema wahurumeni walio ardhini na atawahurumia alie mbinguni,na sifa ya rehma ni katika sifa za mwenyezi mungu alie tukuka,na mbwana mtume muhammad s.a.w alikuwa nimwingi wasikitiko na ruhuma kwa umma wake wote
Khutba ya

Mwenyezi Mungu anasifika kwa sifa ya rehema kwa watu wake mwenye kurehemu na mwingi wa huruma. Ni sifa mbili za Mwenyezi Mungu, mwingi wa huruma kwa viumbe vyote hapa duniani, na kwa waumini siku ya kiyama, mwenye rehema pekee siku ya kiyama. Rehema zake Mwenyezi Mungu hazihesabiki, amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال الله تعالى): مَا يَفْتَحِ اللَّهُ لِلنَّاسِ مِنْ رَحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِنْ بَعْدِهِ) [فاطر: 2]

{{Rehema anayoifungua Mwenyezi Mungu kwa watu, hakuna wa kuizuia; Na Anayozuia hakuna wa kuipeleka mbele}}.

Amesema Shinqiti: rehema zake Mwenyezi Mungu ni kwa watu wote duniani na kesho akhera kama kuteremsha mvua. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى (فَانْظُرْ إِلَى آَثَارِ رَحْمَةِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ([الروم: 50]

{{Basi ziangalie alama za rehma ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake}}. Enyi Waja wa Mwenyezi Mungu, sisi tunatakiwa tuwe na rehema kati yetu, na baina ya viumbe vyote, kwasababu tofauti kama:-

Mwenyezi Mungu ametuamrisha kama alivyosema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): “Kuweni na rehema mtarehemewa, sameheni mtasahemewa”

Tukisifika na tabia hii tutapata watakaoturehemu katika dunia. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Warehemuni walio duniani mtarehemewa na walio mbinguni]. Na amesema tena Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Asiyerehemu watu, Mwenyezi Mungu pia nae hamrehemu].

Sampuli za Rehema za Mwenyezi Mungu

Kuwaumba wanadamu kwa sura nzuri, Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ) [التين: 4]

{{Bila shaka tumemuumba mwanadamu kwa umbo lililo bora kabisa}}.

Kumtukuza mwanadamu na kumfadhilisha kuliko viumbe vyote. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال) : وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آَدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى كَثِيرٍ مِمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا) [الإسراء: 70]

{{Kwahakika tumewatukuza wanadamu na tumewapa ya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba, kwa utukufu ulio mkubwa}}.

Kumpatia mwanadamu riziki, Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال تعالى) : وَمَا مِنْ دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُبِينٍ) [هود: 6]

{{Na hakuna nyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Mwenyezi Mungu. Na Anajua makao yake ya milele, na mahali pa kupita tu. Yote yamo katika kitabu kinachodhihirisha}}.

Kudhalilisha vilivyomo mbinguni na ardhini kwa ajili yetu, amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :

قال تعالى): وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآَيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ) [النحل: 12]

{{Na amekutiisheni usiku na mchana, na jua na mwezi. Vyote vimeumbwa kwa ajili ya maslahi yenu. Na pia nyota zimetiishwa kwa amri yake}}.

Kutumilizwa Mtume na kubainishia watu pepo na kuwakhofisha na moto, amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنْزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ وَأَنْزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ [الحديد: 25] ( {{Kwahakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili waziwazi na Tukateremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu}}.

Kutumilizwa kwetu Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

و قال): رُسُلًا مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ) [النساء: 165]

{{Nasi hatukukutuma, ila uwe rehema kwa walimwengu wote}}.

Kupewa sheria ya kiislamu, na sheria yenyewe ni nyepesi. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Fanyeni upesi wala msifanye uzito, na wabashirieni watu wala msiwakhofishe]. Ndugu Waislamu, tufanye bidii kufanya mambo ya kheri ili tupate rehema za Allah. Rehema za Allah hazipatikani kwa kutamani bali ni lazima Muislamu kufuata sababu zote zitakazo mfiksha yeye kupata rehema za Mwenyezi Mungu.

Khutba ya pili

Rehema ya kutumilizwa Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)

Mtume Muhammad Ametumilizwa kwa wanadamu wote akiwa ni rehema kwao. Ameshuhudia Mwenyezi Mungu rehema ya kutumiliza Mtume wetu Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Kwa kusema (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى : (لقد جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُمْ بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ) [التوبة: 128] {{Kwahakika amekufikieni Mtume aliye jinsi moja na nyinyi, yanamuhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni. Na kwa walioamini ni mpole na mwenye huruma}}.

Sura za Rehema za Mtume wetu Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)

Pamoja na maadui zake, alienda Twaif kuwalingania, walimpiga mawe mpaka akatokwa na damu na wakamtukana hapo Mwenyezi Mungu alimpeleka Malaika wa jabali akasema ukitaka niwafunike na jabali nitafanya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: [Usifanye huenda wakatokea katika watoto wao mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu].

Tukio moja la bedui kukojoa Msikitini na maswahaba wakataka kumpiga, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akawakataza na kusema mwacheni amalize mkojo wake na baada ya hapo akamuambia [ Msikiti umejengwa kumuabudu Mwenyezi Mungu].

Ni mpole mno

Anakuja mtu na kumshika Mtume wa Mwenyezi Mungu mabegani kwa nguvu na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) anamgeukia na kumwangalia kwa tabasamu.

Mtu anamkopesha Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na anakuja kudai deni lake kabla ya wakati wake na kusema: [Enyi watu wa Abdul Mutwalib mnachelewesha kulipa madeni, mpaka maswahaba wanataka kumpiga mtu huyo, na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema “Mwenye haki ana haki ya kusema”].

Pamoja na waumini, amepokea Malik bin Huweinth akisema: “Tumekaa kwa Mtume siku ishirini akadhani kuwa tunawatamani watu wetu, akatuuliza kuhusu hali zao, tukamfahamisha akasema nendeni mkawafundishe kuswali kama mnavyoniona nikiswali pamoja na kuadhini na kukimu”.

Kiongozi wa Kiislamu Kuwa na Rehema

Mtume wa Mwenyezi Mungu amemuomba Mwenyezi Mungu yoyote atakaye shika madaraka katika nchi akisema: [Atakaye shika madaraka katika umma wangu na kuwa na huruma basi Mwenyezi Mungu pia huwa na huruma, na atakae wafanyia uzito umma wangu basi Mwenyezi Mungu pia atamfanyia uzito]. Uongozi si utukufu bali ni ukalifishaji. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kumwambia Aba Dharr: [Uongozi ni amana, na siku ya Qiyama ni majuto, isipokuwa kwa atakayechukua uongozi huo kwa haki, na kupeana haki hiyo].

Viongozi wema waliotangulia walikuwa walikuwa wakifuatilia hali za watu wao, ‘Umar Bin Khattab alikuwa akienda kwa mwanamke mzee kipofu akisafisha mkojo wake na choo, na kumpelekea chakula ‘Umar akaona kuwa kuna mtu anayemtangulia katika kumhudumia mama huyo mzee, akamkuta ni Abubakar ambaye alikuwa ni kiongozi wa Kiislamu.

Kuwarehemu Wanyama

Kuna baadhi za hali imeharamishwa kuwafanyia wanyama:-

Kumfunga mnyama: Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Ameingia mwanamke motoni kwa ajili ya paka aliyemfungia bila ya kumlisha, na kutomuacha kula wadudu katika ardhi].

Kuwapiganisha wanyama: Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amekataza kuwapiganisha wanyama.

Kuuwa wanyama bila ya sababu (mchezo). Neno lake Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : [Ndege anadai haki yake mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama kuuliwa bila ya sababu].

Kufanya hisani katika kuchinja wanyama. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Mkichinja fanyeni wema na mtie kisu makali].

Mwisho

Ndugu Muislamu, ili tuweze kupata rehema za Mwenyezi Mungu, ni wajibu juu yetu kutekeleza sababu zifuatao:-

Kubadilika kutoka hali moja na kwenda katika hali nyingine ni njia moja ya kupata rehma za Mwenyezi Mungu. Mfano kutembelea mayatima na kuwasaidia, kujua hali za maskini wasio jiweza.

Kujuwa malipo makubwa watakaopata wenye kupata rehema za Mwenyezi Mungu

Kuwaheshimu wazazi na kila mtu ambaye ni mkubwa wako kwa umri.

Tunamuomba Allah Atufinike kwa rehma zake hapa duniani na kesho siku ya mwisho.

 





Vitambulisho: